Tabibu
mtu anaye elimu ya tiba / From Wikipedia, the free encyclopedia
Tabibu (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: physician) ni mtu aliyesoma elimu ya tiba hadi kufikia kiwango kinachompa uwezo wa kutambua na kutibu magonjwa mbalimbali.
Tabibu anashirikiana na watu wengine waliojifunza sehemu za elimu ya afya na tiba kama vile wauguzi, wataalamu wa tibamaungo, tibaredio au uchunguzi wa maabara, wafamasia na wengineo. Kutokana na elimu yake ya juu tabibu ni yule anayefanya maamuzi kuhusu mwelekeo na matibabu na chaguo la dawa.
Kwa kawaida tabibu anatakiwa kutimiza masomo ya tiba kwenye chuo kikuu kwa miaka kadhaa. Masomo hayo ni pamoja na au yanafuatwa na vipindi vya kupata maarifa ya kazi akimsaidia tabibu mzoefu katika hospitali. Matabibu wengi wanaendelea kusoma elimu kwenye fani za pekee kama vile upasuaji, jinakolojia, tiba ya watoto, magonjwa ya akili na mengine.