![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/2d/Suni-Tygerberg_Zoo.jpg/640px-Suni-Tygerberg_Zoo.jpg&w=640&q=50)
Suni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Suni | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Dume la suni mashariki (Neotragus moschatus) | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 2, spishi 3, nususpishi 4:
| ||||||||||||
Suni ni wanyamapori wadogo sana wa jenasi Neotragus na Nesotragus katika familia Bovidae. Wanyama hawa ni wadogo kabisa wa Bovidae (kimo sm 25–40 begani, urefu sm 40–60 na uzito kg 2.5–5.5). Wanatokea misitu minyevu na mikavu ya Afrika kusini kwa Sahara yenye kichaka kizito. Dume ana pembe fupi kwa urefu wa sm 3.5 hadi 13 kuhusiana spishi. Rangi yao ni kahawianyekundu lakini nyeupe upande wa chini. Suni hula majani, macho ya maua, machipukizi, nyoga, manyasi na mimea.
Zamani spishi zote ziliainishwa katika jenasi Neotragus lakini uchunguzi wa ADN ulifunua kwamba spishi hizi hazina nasaba kwa karibu. Suni mdogo labda ana nasaba na paa (Cephalophinae) huku spishi mbili nyingine zikiwa na nasaba na swala (Antilopinae).