Ndegejinga
Familia wa ndege wakubwa wa bahari / From Wikipedia, the free encyclopedia
Ndegejinga ni ndege wakubwa wa bahari wa familia Sulidae. Wana domo refu na mabawa marefu yaliyochongoka. Takriban spishi zote wana mwili mweupe na viasi mbalimbali vya nyeusi kwa mabawa na mkia. Spishi kadhaa zina namna kahawia na ndegejinga tumbo-jeupe ana rangi ya kahawa nzito na tumbo jeupe. Ndege hawa hupiga mbizi kutoka urefu mkubwa ili kukamata samaki au ngisi. Huzaa ndani ya makoloni makubwa. Jike hutaga yai moja au mayai mawili, lakini kinda atokaye kwanza katika yai lake amsukuma ndugu wake mdogo nje ya tundu. Huyu afa kwa njaa au aliwa na ndege wa aina nyingine.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Ndegejinga | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Ndegejinga kinyago | ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 3:
| ||||||||||
Funga