Sosholojia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sosholojia ni fani ya sayansi inayochunguza mwenendo wa kijamii, yaani binadamu katika maisha ya jamii: unavyoanza, unayoendelea, unavyojipanga na unavyosababisha miundo.[1]
Kwa maneno mengine, sosholojia inamsoma mtu katika mahusiano yake: mtu na mtu, mtu na watu (kundi) na hivyo huweza kugundua tabia zake mbalimbali.
Somo hilo linahusiana na masomo mengine, kama vile anthropolojia, historia, saikolojia na uchumi.
Ni mojawapo kati ya sayansi za jamii nayo inatumia mbinu tofauti za kutambua hali halisi, halafu inazichunguza kimpango.