![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/5/5d/Original_laws_of_the_game_1863.jpg/640px-Original_laws_of_the_game_1863.jpg&w=640&q=50)
Sheria za soka
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sheria za soka (kwa Kiingereza: “The Law Of the Game”; kifupi: LOTG[1]) ni kanuni zilizoundwa maalumu ili kusimamia masuala yote yanayohusu mchezo wa soka.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/5/5d/Original_laws_of_the_game_1863.jpg/640px-Original_laws_of_the_game_1863.jpg)
Sheria inaelezea idadi ya wachezaji kila timu inapaswa kuwa nao, urefu wa mchezo, kipimo cha uwanja na mpira, asili na aina za faulu refa anazoweza kutoa adhabu, sheria yenye utata kuliko zote ya kuotea na sheria nyingine kadhaa. Wakati wote wa mchezo, ni jukumu la refa kufafanua na kutekeleza kwa jinsi sheria inavyoelekeza.
Katikati ya karne ya 19, kulifanyika jaribio ya kugeuza sheria kuwa za ishara zaidi. Sheria hizi zina historia ya kuanzia mwaka 1863 ambapo kifungu cha sheria kiliundwa na bodi iliyokua ikishughulikia masuala ya soka iliyoundwa mwaka huohuo kwa jina la (The Football Association|Footba). Kwa muda mrefu sheria hizo zimekua zikirekebishwa na kuanzia mwaka 1886 ziliwekwa chini ya bodi maalumu (International Football Association Board).
Ndio sheria pekee ambazo FIFA wameruhusu zitumike nan chi wanachama wake.[2] Sheria hizi zinaruhusu utofauti mdogo baina ya nchi.