Saint-Pierre na Miquelon (kwa Kifaransa: Saint-Pierre-et-Miquelon) ni eneo la ng'ambo la Ufaransa (Collectivité d'outre mer) ambalo ni funguvisiwa karibu na pwani ya Kanada katika bahari ya Atlantiki.
| |||
Wito: A mare labor (Kazi kutoka bahari) | |||
Lugha rasmi | Kifaransa | ||
Mji Mkuu | St. Pierre | ||
Rais wa Halmashauri Kuu | Stéphane Artano | ||
Mkuu wa Mkoa (Préfet) | Albert Dupuy | ||
Eeno – Jumla – % maji |
242 km² 0.0% | ||
Idadi ya wakazi – Jumla (2011) |
6,080 | ||
Pesa | Euro (€;EUR) | ||
Jamla la pato la eneo (Wanazaa kiasi gani cha mali kwa mwaka) | $48.3 Millioni | ||
Kanda la saa | UTC-3 | ||
Simu ya eneo | 508 ¹ | ||
Intaneti TLD | .pm | ||
1. 0508 kutoka Ufaransa bara. | |||
Jiografia
Funguvisiwa liko karibu na jimbo la Newfoundland la Kanada.
Visiwa vikubwa zaidi ni Saint-Pierre (km² 26), Miquelon (km² 110), Langlade (km² 91) halafu kuna visiwa vingine vidogo . Miquelon na Langlade vilikuwa visiwa viwili lakini leo vimeungwa kwa kanda ya nchi kavu vyaitwa pamoja kama "Miquelon". Jumla la eneo ni km² 242 lenye wakazi 6,316 (Saint-Pierre: wakazi 5.618, Miquelon na Langlade: wakazi 698).
Karibu wote wanaongea Kifaransa na ni waamini wa Kanisa Katoliki.
Historia
Visiwa vimetembelewa na wavuvi kutoka Ulaya tangu karne ya 15.
Inaaminiwa ya kwamba makazi ya kwanza ya kudumu ya wavuvi Wafaransa yalianzishwa katika karne ya 17.
Tangu vita ya miaka saba visiwa hivi vilikuwa mabaki pekee ya koloni la Kanada ya Kifaransa.
Visiwa hii ni mabaki ya koloni kubwa la zamani lililoitwa "Nouvelle-France" (Ufaransa Mpya) na kuenea katika Kanada.
Uchumi
Uchumi umetegemea tangu mwanzo uvuvi. Siku hizi kuna pia utalii.
Siasa
Wakazi wa visiwa ni raia wa Ufaransa. Huchagua bunge lao lenye watu 19. Bunge la eneo linamchagua mwakilishi mmoja katika bunge la kitaifa la Ufaransa.
Saint-Pierre na Miquelon si sehemu ya Eneo la forodha la Ulaya.
Viungo vya nje
- Official tourism website for St Pierre and Miquelon
- Tourism ressources and information
- Le Phare: Association of Tourism Professionals
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.