Philippus Mwarabu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Marcus Julius Philippus (takriban 204 – Septemba 249) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia Februari 244 hadi kifo chake. Alipenda Ukristo.
Alimfuata Gordian III akauawa na mwandamizi wake, Gaius Messius Quintus Decius ambaye alianza mapema dhuluma mpya dhidi ya Wakristo.
Aliitwa Mwarabu kwa vile alizaliwa na wazazi Waarabu katika jimbo la Arabia karibu na mji wa Damasko (Syria).