Kengewa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kengewa ni ndege mbua wa jenasi mbalimbali za nusufamilia Perninae katika familia Accipitridae. Wana mabawa marefu na mkia mrefu mwenye miraba myeusi. Spishi za jenasi Henicopernis na Pernis hula nyuki, nyigu na asali hasa lakini spishi nyingine hula wanyama wadogo. Hujenga tago lao juu ya mti msituni.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Kengewa | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kengewa mlanyuki | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 6 za kengewa:
| ||||||||||||
Funga
Mpaka juzi kengewa mlanyuki tu ameonwa Afrika kusini kwa Sahara, lakini mwaka 2005 kengewa wa Asia ameonwa huko Gaboni.