Kipepeo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Vipepeo ni wadumili (hali ya mwisho ya metamofosisi) wa wadudu wa oda ya Lepidoptera.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Kipepeo | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Papilio antimachus, kipepeo mkubwa kabisa wa Afrika | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Familia za juu 2, familia 7:
| ||||||||||||
Funga
Jinsi ilivyo kwa wadudu wengi maisha ya kipepeo huanza kama yai. Anatoka kwenye yai kwa umbo la kiwavi. Baada ya miambuo minne kiwavi huwa bundo. Ndani ya bundo hugeuka kuwa kipepeo anayetoka na kutaga mayai tena. Mzunguko huu kwa jumla unaitwa metamofosisi.
Vipepeo huishi kwa muda mfupi. Hula kiowevu pekee, hasa cha mbochi wa maua.