Nusuranyota (kwa kiingereza: quasar) ni kiini angavu sana cha majarra hai. Nguvu ya mnururisho wake inatokana na shimo jeusi la tungamomno, lenye tungamo kutoka tungamo ya Jua milioni kumi hadi bilioni kumi, na huzingirwa na kisahani cha uongezekaji. Kuanguka kwa gesi ya kisahani hupasha joto na hutoa nishati yenye jinsi ya mnururisho sumakuumeme. Nishati ng’avu ya nusuranyota ni kubwa mno; nusuranyota zenye nguvu zaidi zina mng’aro maelfu ya mara mkubwa kuliko majarra kama Njia Nyeupe.[1][2] Nusuranyota huainizishwa kama kijamii cha jamii kubwa zaidi ya kiini cha majarra hai. Misogeo miekundu ya nusuranyota inatokana na kuvimba kwa Ulimwengu.[3]

Thumb
Picha ya sanaa ya kisahani cha uongezekaji cha nusuranyota.

Istilahi nusuranyota ni ambatani ya nusura na nyota. Kwa kiingereza, quasar ni mkato wa “quasi-stellar radio source”—kwa sababu zilitambuliwa kwanza wakati wa miaka ya 1950 kama violwa vya asili isiyojulikana ambavyo hutokeza mawimbiredio—na zilipochunguzwa kwa masafa wa mawimbi yanayoonekena, zilifanana na nukta dhaifu ya nuru kama nyota. Taswira za mwonekano wa juu za nyota, hasa kutoka Darubini ya Angani ya Hubble, zimeonyesha kwamba nusuranyota ziko katika vitovu vya majarra, na majarra nyingine zinaingiliana sana au zinachanganyana.[4]

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.