![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/1b/Nokia1100_new.jpg/640px-Nokia1100_new.jpg&w=640&q=50)
Nokia 1100
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nokia 1100 ni simu madhubuti iliyotengenezwa na Nokia. Imelengewa nchi ambazo bado zinaendelea na watumizi ambao hawahitaji vifaa vingi kwenye simu zao ila ya uwezo wa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi, saa, n.k.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/1b/Nokia1100_new.jpg/640px-Nokia1100_new.jpg)
Simu ya 1100 inafanana na Nokia 3210/Nokia 3310 ambazo zilikuwa simu maarufu katika miaka iliyopita kabla ya uzinduzi mpya wa vifaa vya simu kama kamera.
Zaidi ya nakala milioni 200 za simu hii zimeuzwa tangu ilipoanzishwa mnamo 2003, na kuifanya iwe simu iliyopata mauzo mazuri zaidi kote duniani.[1] Hata hivyo, ilishinda mauzo ya Playstation 2 iliyouza nakala milioni 138 na simu ya Motorola RAZR iliyouza nakala milioni 120.).[2]