Ngurunguru
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ngurunguru au mbuzi mawe (Oreotragus oreotragus) ni swala wadogo wanaotokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Jina “mbuzi mawe” ni kielekezi cha makazi yao: maeneo yenye mawe na majabali mengi. Swala hawa ni wadogo wenye kimo cha sm 58 begani. Wana rangi ya kahawa hadi kijivu, karibu na zaituni, na vidoa vidogo vingi. Rangi hii inafanana na rangi ya majabali ambapo wanaishi na kwa sababu ya hii hawaonekani vizuri kutoka umbali mkubwa. Madume wana pembe za sm 10–15. Katika Afrika ya Mashariki majike wana pembe pia mara nyingi. Wanyama hawa wasimama kwa ncha za kwato zao na wanaweza kubana kwato nne zote juu ya kipande cha jabali kwa upana wa sarafu kubwa. Hula mimea inayomea kati ya majabali. Hawana haja ya kunywa, kwa sababu hupata maji ya kutosha kutoka chakula chao.
Ngurunguru | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Dume la ngurunguru (Oreotragus oreotragus) | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Nususpishi 11:
| ||||||||||||||||||
Msambao wa ngurunguru | ||||||||||||||||||
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ngurunguru kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.