Neptuni (elementi)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Neptuni ni elementi katika mfumo radidia yenye alama Np. Namba atomia ni 93 na uzani atomia ni 237. Jina limechaguliwa kutokana na sayari Neptun.
Ukweli wa haraka Neptuni (neptunium) ...
Neptuni (neptunium) | |
---|---|
Atomi ya Neptuni | |
Jina la Elementi | Neptuni (neptunium) |
Alama | Np |
Namba atomia | 93 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 237 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 22, 9, 2 |
Densiti | 20.25 g·cm³ |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 910 K (637 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 4273 K (4000 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 4 · 10-17 % |
Hali maada | mango |
Funga
Neptuni ni metali na elementi ya tamburania. Kwa sababu hii haipatikani duniani kiasili isipokuwa kwa kiwango kidogo sana pamoja na plutoni ndani ya mawe ya mtapo wa urani. Inatokea katika tanuri nyuklia.
Ikiwa elementi tamburania muda wa nusumaisha si mrefu sana. Isotopi ya 237Np ina nusumaisha ya miaka milioni mbili. Lakini isotopi ya 235Np ina nusumaisha ya siku 396 tu.
Rangi ya Neptuni ni ya kifedha. Ina unururifu hivyo pamoja na muda wake wa nusumaisha yafaa kwa matumizi ya mabomu ya kinyuklia.