![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/21/Ptolemy_I_Soter_Louvre_Ma849.jpg/640px-Ptolemy_I_Soter_Louvre_Ma849.jpg&w=640&q=50)
Nasaba ya Waptolemaio
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kuhusu mtaalamu mashuhuri wa karne ya 2 BK angalia Klaudio Ptolemaio
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/21/Ptolemy_I_Soter_Louvre_Ma849.jpg/640px-Ptolemy_I_Soter_Louvre_Ma849.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/bc/Ptolemaic-Empire-300BC.jpeg/640px-Ptolemaic-Empire-300BC.jpeg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/4c/Posthumous_painted_portrait_of_Cleopatra_VII_of_Egypt%2C_from_Herculaneum%2C_Italy.jpg/640px-Posthumous_painted_portrait_of_Cleopatra_VII_of_Egypt%2C_from_Herculaneum%2C_Italy.jpg)
Nasaba ya Waptolemaio (Kigiriki Πτολεμαῖοι, Ptolemaioi) walikuwa mlolongo wa watawala wa Misri ya Kale na familia zao tangu mwaka 305 KK hadi mwaka 30 BK [1]. Waptolemaio walikuwa familia yenye asili ya Kigiriki katika Masedonia. [2] [3] [4] [5] [6] Walikuwa nasaba ya mwisho ya Misri ya Kale wakitawala juu ya Milki ya Kiptolemaio.
Nasaba ilianzisha na Ptolemaio I aliyewahi kuwa rafiki wa karibu na jenerali wa Aleksander Mashuhuri. Baada ya kifo cha Aleksander kwenye mwaka 323 KK aliteuliwa kuwa gavana wa Misri. Mnamo 305 KK alijitangaza kuwa mfalme Ptolemaio I akijulikana pia kwa jina la nyongeza kama Sōter ("mwokozi"). Familia ya Ptolemaio ilitawala Misri hadi wakati ushindi wa Warumi kwenye mwaka 30 KK.
Kiutamaduni Waptolemaio walikuwa Wagiriki lakini walijitahidi kutumia mapokeo ya Misri kwa utawala wao. Walikaa katika mji mkuu Aleksandria uliokuwa pia mji wenye ustaarabu wa Kigiriki ulioundwa na Aleksander Mashuhuri mwenyewe alipovamia Misri kwenye mwaka 332/331 KK. Malkia wa mwisho Kleopatra alikuwa Mptolemaio wa kwanza aliyeongea Kimisri fasaha.
Katika karne ya pili ya utawala wao walirudi katika mji mkuu wa kale Memphis kwa ibada ya kupokea ufalme na taji la Misri kila baada ya kifo cha mfalme na kuingia mfalme mpya.
Walipokea pia desturi ya Kimisri kwamba farao aliweza kuoa dada yake [7] na Waptolemaio wengi walizaliwa katika ndoa za aina hiyo.
Mafarao, yaani watawala wa kiume, walitumia jina rasmi "Ptolemaio" na tangu mwaka 193 KK malkia wote walitumia jina "Kleopatra" lililo mashuhuri hasa kutokana na malkia wa mwisho, Kleopatra VIII aliyefariki wakati wa uvamizi wa Kiroma akiwa mtawala wa mwisho wa Misri huru na wa nasaba yake.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/06/Cammeo_gonzaga_con_doppio_ritratto_di_tolomeo_II_e_arsinoe_II%2C_III_sec._ac._%28alessandria%29%2C_da_hermitage.jpg/640px-Cammeo_gonzaga_con_doppio_ritratto_di_tolomeo_II_e_arsinoe_II%2C_III_sec._ac._%28alessandria%29%2C_da_hermitage.jpg)