Namba isiyowiana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Namba isiyowiana (kwa Kiingereza: en:irrational number[1]) ni namba halisi ambayo haiwezi kuonyeshwa kama wianisho safi baina ya nambakamili.
Mifano mashuhuri ni kipeuo mraba cha 2 na namba ya duara π (Pi). Kwa mfano Pi ikiandikwa kwa namna ya desimali inaanza hivi 3.14159265358979 .... lakini haiwezi kamwe kuonyeshwa kikamilifu kwa kuongeza tarakimu baada ya nukta.