Mvua ya wanyama
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mvua ya wanyama ni tukio la nadra sana ambapo wanyama wadogo huanguka kutoka angani.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/2b/Singapourfish.jpg/220px-Singapourfish.jpg)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/0f/Wea02218_-_Flickr_-_NOAA_Photo_Library.jpg/640px-Wea02218_-_Flickr_-_NOAA_Photo_Library.jpg)
Matukio kama hayo yameripotiwa mara kwa mara katika nchi nyingi katika historia. [1] Wanyama wanaotajwa katika matukio hayo ni hasa samaki, chura na ndege.
Taarifa ziko nyingi kiasi kwamba wataalamu wanakubali ni kweli lakini hadi sasa haikuwezakana kuzifanyia utafiti kamili[2].
Kati ya maelezo yaliyopendekezwa kuna dhana kwamba vimbunga vinaweza kuchukua viumbehai kama vile samaki au vyura, na kuwainua juu hadi kilomita kadhaa. [3] [4]