Mto Marne
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Marne ni mto wa Ufaransa, tawimto upande wa kulia wa Seine katika eneo la mashariki na kusini ya Paris. Una urefu wa kilometre 514 (mi 319).[1] Mto ulizipatia jina lake wilaya za Haute-Marne, Marne, Seine-et-Marne, na Val-de-Marne.
Chanzo | Grand Est |
Mdomo | Seine 48°48′57″N 2°24′40″E |
Urefu | 514 km |
Mto Marne unaanza katika platuu ya Langres, unatiririka kuelekea kaskazini, kisha unaelekea magharibi kati ya Saint-Dizier na Châlons-en-Champagne, na kuungana na Seine katika Charenton katika Paris. Katika kanda la Champagne sehemu ya maji huongozwa katika ziwa la kujengwa na binadamu la Lac du Der-Chantecoq, ili kudhibiti mtiririko wa maji. Kwa njia hiyo kiwango cha maji cha chini huzuiwa.[2]
Mto Marne ulikuwa eneo la mapigano mawili wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. La kwanza Lilikuwa mgeuko wa Vita vya Kwanza vya Dunia katika mwaka wa 1914. La pili lilitokea miaka minne baadaye, katika mwaka wa 1918.
Katika karne ya 19 na 20, Marne ulipendeza wachoraji na wasanii wengi; miongoni mwao ni:
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.