From Wikipedia, the free encyclopedia
Abuna Yosef ni mlima maarufu ulio karibu na mwinuko wa mashariki wa Nyanda za Juu za Ethiopia. Una urefu wa mita 4,260 (futi 13,976) juu ya usawa wa bahari. Ni mlima wa sita kwa urefu nchini Ethiopia na mlima wa 19 kwa urefu barani Afrika. Unapatikana sehemu inayojulikana kama Lasta Massif katika eneo la Semien Wollo, Mkoa wa Amhara.
Kitu kinachojulikana sana kwenye mlima huo ni Kanisa la Gennete Maryam, kanisa lililochongwa mwambani ambalo liliripotiwa kuwa kanisa la mila lilifutwa wakati wa utawala wa Yekuno Amlak. [1]
Pia makanisa manne yaliyokuwa yakijitegemea yalijengwa ndani ya mapango ya mlima, kanisa kongwe na maarufu zaidi lilikuwa ni Kanisa la Yemrehana Krestos, lililojengwa na mfalme wa Zagwe (Mfalme wa jina moja). Matatu mengine ni Emakina Medhane Alem (linakisiwa huenda lilijengwa na Yekuno Amlak mwishoni mwa karne ya 13), Lidetta Maryam na Zammadu Maryam (nayo yanakisiwa huenda yalijengwa karne ya 15). [2] Makanisa ya Lalibela yapo katika sehemu za chini za milima.
Sehemu ya Uhifadhi wa mlima huu hupatikana Jamii ya Abuna Yosef inajumuisha kilomita za mraba 70 za ngome ya Abuna Yosef. [3]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.