Menofisi ni spishi za nyoka za jenasi Lycophidion katika familia Lamprophiidae. Jina lao linatoka kwa nususi kwamba meno yao ni marefu na yamepindika nyuma.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Menofisi |
Menofisi wa Rasi (Lycophidion capense) |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Nusufaila: |
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
|
Ngeli: |
Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
|
Oda: |
Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
|
Nusuoda: |
Serpentes (Nyoka)
|
Oda ya chini: |
Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
|
Familia: |
Lamprophiidae (Nyoka walio na mnasaba na chata) Fitzinger, 1843 |
Nusufamilia: |
Lamprophiinae (Nyoka wanaofanana na chata) Fitzinger, 1843 |
Jenasi: |
Lycophidion Fitzinger, 1843 |
|
Ngazi za chini |
Spishi 20:
- L. acutirostre Günther, 1868
- L. albomaculatum (Steindachner, 1870)
- L. capense (Smith, 1831)
- L. depressirostre Laurent, 1968
- L. helmichi Laurent, 1964
- L. irroratum (Leach, 1819)
- L. laterale Hallowell, 1857
- L. meleagre (Boulenger, 1893
- L. multimaculatum Böttger, 1888
- L. namibianum Broadley, 1991
- L. nanum (Broadley, 1958)
- L. nigromaculatum (W. Peters, 1863)
- L. ornatum Parker, 1936
- L. pembanum Laurent, 1968
- L. pygmaeum Broadley, 1996
- L. semiannule W. Peters, 1854
- L. semicinctum A.M.C. Duméril, Bibron & Duméril, 1854
- L. taylori Broadley & Hughes, 1993
- L. uzungwense Loveridge, 1932
- L. variegatum Broadley, 1969
|
Funga
Nyoka hawa ni wafupi. Majike ya spishi kadhaa yanaweza kufika sm 60 lakini madume ni wafupi zaidi na menofisi wengi ni kati ya sm 20 na 45. Kichwa chao ni bapa. Kwa kawaida rangi yao ni kijivu au kahawia na mara nyingi wana madoa.
Menofisi hupumzika mchana katika vishimo. Huwinda usiku na kukamata mijusi kwa meno yao yaliyopindika.
Nyoka hawa hawana sumu na hawaihitaji kwa sababu wanakula mijusi tu. Wakishikwa na watu hawang'ati kwa kawaida, lakini tahadhari kwa sababu nyoka wachimbaji fulani wanafanana na menofisi na hawa hung'ata na huwa na sumu, ingawa hawawezi kuua mtu mzima.