From Wikipedia, the free encyclopedia
Mchezo wa pool (kwa Kiingereza "Pool" au "Billiards") ni mchezo ambao unachezwa na watu wawili au hata zaidi kwa kutumia mipira minane ya rangi pamoja na mpira mmoja mweupe, pia na fimbo ndefu.
Mchezo huchezwa sana katika nchi za Ulaya na Australia, uwanja wake una vitundu au mifuko sita au nane kwa ajili ya kuingizia mpira.
Mchezo wa pool ni kati ya michezo inayopendwa sana na vijana. Pool huwa na bodi yenye vijishimo ambapo vijana hupiga vijipira kwa miti huku lengo lao likiwa kuweka mipira yote kwa vishimo. Kila mchezaji hujaribu kila awezalo kuhakikisha kwamba yeye ndiye atakayerusha mipira mingi zaidi ndani ya vile vijishimo.
Kwa jamii nyingi, mchezo huu wa pool huchezwa katika vilabu, au hata madukani penye vijana wengi na wazee. Wachezaji wengi wa pool hutumia pesa ili kwamba atakayeshinda katika pool anashinda tita la pesa.
Ili uweze kuibuka mshindi wa pool, lazima uwe na jiti zuri (yaani cue stick) ambayo itaweza kurusha mipira kwa urahisi.
Yafaa pia bodi ya pool iwe nzuri yenye kitambaa chororo ili kwamba iwe rahisi kwa mipira kubingirika hadi kwenye vishimo.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Mchezo wa pool kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.