Kwa mfalme au mwene mkuu wa kwanza wa Washambaa tazama "Mbegha"
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Mbega |
Mbega mweupe kusi |
Uainishaji wa kisayansi |
Domeni: |
Eukaryota (Viumbe walio na seli zenye kiini)
|
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Ngeli: |
Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
|
Oda: |
Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
|
Nusuoda: |
Haplorrhini (Wanyama wanaofanana kiasi na kima)
|
Oda ya chini: |
Simiiformes (Wanyama kama kima)
|
Familia ya juu: |
Cercopithecoidea
|
Familia: |
Cercopithecidae (Wanyama walio na mnasaba na kima)
|
Nusufamilia: |
Colobinae (Mbega)
|
Jenasi: |
Colobus Illiger, 1811
Nasalis E. Geoffroy, 1812
Piliocolobus Rochebrune, 1877
Presbytis Eschscholtz, 1821
Procolobus Rochebrune, 1877
Pygathrix E. Geoffroy, 1812
Rhinopithecus Milne-Edwards, 1872
Semnopithecus Desmarest, 1822
Simias Miller, 1903
Trachypithecus Reichenbach, 1862
|
|
Funga
Mbega (pia: mbegha [1] ) ni kima wa nusufamilia Colobinae katika familia Cercopithecidae. Wanatokea Afrika na Asia.
Spishi nyingi huishi mitini lakini spishi nyingine huishi savana zenye miti na hata mijini. Vidole gumba vya spishi za Afrika vimekuwa vigutu pengine ili kurahisisha kwenda katika miti. Mbega hula majani, maua na matunda, pengine wadudu na wanyama wadogo.
- Colobus angolensis, Mbega Mweupe Kusi (Southern Black-and-white Colobus)
- Colobus guereza (=abyssinicus), Mbega Mweupe Mashariki, Kuluzu au Dolo (Eastern black-and-white colobus)
- Colobus polykomos, Mbega Mfalme (King Colobus)
- Colobus satanas, Mbega Mweusi (Black Colobus)
- Colobus vellerosus, Mbega Mapaja-meupe (White-thighed Colobus)
- Piliocolobus badius, Mbega Mwekundu Magharibi (Western Red Colobus)
- Piliocolobus foai, Mbega Mwekundu wa Afrika ya Kati (Central African Red Colobus)
- Piliocolobus gordonorum, Mbega Mwekundu wa Udzungwa (Udzungwa Red Colobus)
- Piliocolobus kirkii, Mbega Mwekundu wa Unguja (Zanzibar Red Colobus)
- Piliocolobus pennantii, Mbega Mwekundu wa Pennant (Pennant's Colobus)
- Piliocolobus preussi, Mbega Mwekundu wa Preuss (Preuss's Red Colobus)
- Piliocolobus rufomitratus, Mbega Mwekundu wa Tana (Tana River Red Colobus)
- Piliocolobus tephrosceles, Mbega Mwekundu wa Uganda (Ugandan Red Colobus)
- Piliocolobus tholloni, Mbega Mwekundu wa Chuapa (Thollon's Red Colobus)
- Procolobus verus, Mbega Kijanikijivu (Olive Colobus)
Mbega mweupe mashariki
Mbega mfalme
Mbega mwekundu magharibi
Mbega mwekundu wa Unguja
Mbega mwekundu wa Uganda
linganisha kamusi kama Websters dictionary; lakini kuna uwezekano wa kwamba tahajia hiyo ni ama kosa la kuchanganya "mbega" = kima na Mbegha= chifu wa kihistoria wa Washambaa au matamshi ya kieneo
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.