From Wikipedia, the free encyclopedia
Ritriti (kutoka Kiingereza "Retreat") ni kipindi cha kujishughulisha na maisha ya Kiroho kwa kujitenga na kazi na mazingira ya kawaida.
Mara nyingi ritriti inaendana na kimya na saumu, ndiyo sababu inaitwa pia "mafungo".
Vipindi vya namna hiyo vinahimizwa katika dini mbalimbali, kama vile Uhindu, Ubuddha, Ukristo na Uislamu.
Kama nafasi ya kukutana na Mungu kwa urahisi na undani zaidi, ya kutafakari neno lake, ya kutulia pengine mbele ya tabenakulo, na hatimaye kuweka maazimio ya kuongoka na kufanya utume, ritriti inaagizwa na Kanisa Katoliki kwa mapadri na watawa, mbali ya kushauriwa kwa walei pia, walau mara kadhaa maishani, kiasi kwamba kuna rehema ya pekee kwa wanaoifanya kila mwezi.
Ritriti ikidumu muda mrefu zaidi inaweza kuitwa mazoezi ya kiroho, hasa ikifuata utaratibu maalumu wa Wajesuiti ulioanzisha na Ignas wa Loyola.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.