Martin Luther King, Jr.
Kiongozi wa haki za binadamu kutoka Marekani (1929-1968) / From Wikipedia, the free encyclopedia
Dr Martin Luther King, Junior (Atlanta, Georgia, 15 Januari 1929 – Memphis, Tennessee, 4 Aprili 1968) alikuwa Mkristo mwenye asili ya Afrika, mchungaji wa Kibaptisti na mwanaharakati mashuhuri kutoka nchi ya Marekani aliyepigania haki za binadamu, hasa Wanegro, wakati nchi hiyo ilipokuwa bado na sheria za ubaguzi wa rangi.
Baadhi ya madhehebu ya Marekani, hasa Waanglikana na Walutheri, yanamheshimu kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe yake ya kuzaliwa au ya kuuawa.