Baptisti ni neno linalotumika pengine kuelezea kinachohusika na mapokeo maalumu ndani ya Ukristo wa Kiprotestanti na hasa kutajia mali au makanisa ya Wabaptisti au madhehebu ya Kibaptisti, ambayo ni kati ya yale yenye waumini wengi zaidi duniani. Wanakadiriwa kuwa milioni 110 katika jumuia 220,000.

Mlango wa kanisa la Kibaptisti huko St. Helier

Mapokeo hayo yamechukua jina lake kutokana na mkazo juu ya imani ya wafuasi wa Yesu Kristo kwamba wanapaswa kuzamishwa ndani ya maji mengi ili kuonyesha imani yao.

Kwa sababu hiyo Wabaptisti hawana desturi ya kutoa ubatizo kwa watoto wachanga.

Mbali ya msimamo huo, Wabaptisti wanatofautiana sana katika teolojia na miundo yao.

Historia

Msimamo wa Kibaptisti ulijitokeza kwanza Uswisi katika karne ya 16, lakini ulipata nguvu zaidi Uingereza katika karne ya 17.

Huko Marekani mwaka 1639 Roger Williams alianzisha kanisa la Kibaptisti mjini Providence, Rhode Island na John Clarke alianzisha kanisa la Kibaptisti mjini Newport, Rhode Island. Haieleweki vyema kanisa gani kati ya hayo lilifunguliwa kwanza. Kumbukumbu za makanisa yote mawili zimepotea.[1]

Mbali na Marekani na Ulaya, siku hizi kuna Wabaptisti wengi hasa Nigeria (milioni 2.5), India (milioni 2.4), Congo (DRC) (milioni 1.9) na Brazil (milioni 1.7).

Tanbihi

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.