Marjorie Oludhe Macgoye
Mwandishi wa Riwaya, Insha na Mashairi / From Wikipedia, the free encyclopedia
Marjorie Oludhe Macgoye (21 Oktoba 1928 - 1 Desemba 2015) alikuwa mwandishi wa riwaya, insha na mashairi.[1] Marjorie Oludhe Macgoye alizaliwa mwaka wa 1928 kama Marjorie Klein mjini Southampton, Uingereza. [1] Alihamia Kenya mwaka wa 1954 na kuolewa na D.G.W. Oludhe-Macgoye 1960 akaingia katika ukoo wake wa Kijaluo.[1] Mwaka wa 1971, alitoa mkusanyiko wa mashairi Poems from East Africa uliokuwa pamoja na "A Freedom Song". [1] Riwaya yake ya mwaka 1986 Coming to Birth ilishinda Tuzo la Sinclair (Sinclair Prize). [1] Alitajwa kuwa "mama wa fasihi ya Kenya". [1] [2]