From Wikipedia, the free encyclopedia
Mama wa Kanisa (kwa Kilatini: Mater Ecclesiae) ni jina la heshima ambalo Bikira Maria amepewa rasmi na Papa Paulo VI tarehe 21 Novemba 1964 wakati wa Mtaguso wa pili wa Vatikano. Jina hilo lilitumiwa kwanza na Ambrosi wa Milano katika karne ya 4[1] halafu na Papa Benedikto XIV mwaka 1748[2], tena na Papa Leo XIII mwaka 1885.[3]
Limeingizwa na Papa Yohane Paulo II katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki[4], hatimaye na Papa Fransisko katika kalenda ya liturujia ya Kanisa la Kilatini siku inayofuata Pentekoste.[5]
Kabla ya hayo yote, sanaa ya Kikristo ilikuwa imezoea kumchora Bikira Maria kati ya Mitume wakati wa kushukiwa na Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste kama ilivyosimuliwa na Mwinjili Luka (Mdo 1-2).
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.