From Wikipedia, the free encyclopedia
Makemake (alama: ;[1] tamka kama ni Kiswahili; jina rasmi: 136472 Makemake) ni sayari kibete inayozunguka jua letu katika umbali mkubwa kwenye ukanda wa Kuiper.
Iligunduliwa na wanaastronomia Michael E. Brown, Chad Trujillo na David Rabinowitz kwenye paoneaanga pa Mount Palomar tarehe 31 Machi 2005.
Jina lilichaguliwa kutokana na mungu muumbaji aliyeitwa "Makemake" katika dini asilia ya Kisiwa cha Pasaka (Easter Island, kwenye Bahari ya Pasifiki). Kuna mapatano katika Umoja wa Kimataifa wa Astronomia kutumia majina ya miungu ya dini mbalimbali kwa magimba yanayoendelea kugunduliwa katika ukanda wa Kuiper. Asili ya jina iko katika lugha ya Kipolinesia na katika dini yao ni muumbaji wa binadamu na mungu wa rutuba. Makemake aliabudiwa kwa umbo la ndege wa bahari. Ishara yake ilikuwa mwanamume mwenye kichwa cha ndege.[2]
Hakuna habari nyingi za uhakika kutokana na umbali wa gimba hili na kwa sababu hadi sasa hakuna chombo cha angani kilichopita karibu nayo. Lakini Makemake inaonekana ni hasa mwamba na barafu ilhali katika baridi iliyopo mbali na jua barafu huwa ngumu kama mwamba.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.