Maeneo ya Shirikisho la Urusi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Maeneo ya Shirikisho la Urusi ni maeneo yanayofanya kikatiba Shirikisho la Urusi. Maeneo haya ni kama majimbo au madola katika nchi nyingine ya shirikisho. Jina la Kirusi ni "субъекты федерации" (subyekti federatsii) inayoweza kutafsiriwa kama "nafsi za shirikisho" au "wanachama wa shirikisho".
Hali halisi yana viwango tofauti sana vya kujitawala kuhusu mammbo ya ndani ama kisiasa, kiuchumi au kiutamaduni. Lakini kila eneo la shirikisho lina wawakilishi 2 katika Halmashauri ya Shirikisho la Urusi ambayo ni kitengo cha juu cha bunge la Urusi.
Katiba ya Urusi inataja aina mbalimbali za maeneo ya shirikisho[1]:
Mwaka 1993 kulikuwa na maeneo mwanachama 89. Idadi hii ilipungua kuwa 83 kwenye mwaka kutokana na kuunganishwa kwa maeneo mbalimbali. Mwaka 2014 mji wa Sevastopol na Jamhuri ya Krim yalikuwa maeneo ya 84b na 85 ya Shirikisho la Urusi ingawa hatua hii haikubaliwa na umma wa kimataifa.