Maada ya giza
From Wikipedia, the free encyclopedia
Katika elimuanga, maada ya giza (kwa kiingereza: dark matter) ni jinsi ya maada ya nadharia tete isiyoingiliana na mnururisho sumakuumeme. Maada ya giza inadokezwa na athari za mvutano zisizoweza kuelezwa vinginevyo na uhusianifu wa jumla kusipokuwa na maada zaidi isiyoonekana. Athari hizi hutokea katika muktadha wa uumbaji wa majarra,[1] lenzi za mvutano,[2] muundo wa ulimwengu kisasa, mwendo wa majarra katika mafungu ya majarra, na anisotropia za mnururisho wa chinichini wa ulimwengu.