From Wikipedia, the free encyclopedia
Ludwig Wilhelm Erhard (* 4 Februari 1897 mjini Fürth; † 5 Mei 1977 mjini Bonn) alikuwa mwanasiasa kutoka nchini Ujerumani.
Erhard alizaliwa akiwa kama mtoto wa mfanyabiashara. Baada ya kumaliza mtihani wake wa kati, akaanza kujifunza masuala uuzaji ili aje kuwa mfanyabiashara. Alijeruhiwa kama mwanajeshi wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya vita, akaanza kusomea masuala ya uchumi katika chuo cha mjini Nuremberg.
Baada ya hapo, akajiendeleza zaidi kusomea masuala ya uchumi katika Chuo Kikuu cha Frankfurt am Main. Baada ya kumaliza masomo yake, akawa anafanya kazi katika kampuni ya baba yake. Baada ya Mdororo Mkuu, kampuni ya baba yake ikafirisika.
Kuanzia 1928 hadi 1942, alikuwa akifanya kazi kama mwanasayansi msaidizi, lakini hakupata changamoto kwa kuwa alikuwa hataki kuwa mmoja kati ya wanajumuia ya Wanazi. Kuanzia 1942 hadi 1945, alikuwa Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Viwanda.
Toka 1949, alifanya kazi na chama cha CDU, lakini sana-sana kwenye 1963. Kuanzia 1945 hadi 1946, alijiunga na serikali ya ugawaji wa Bavaria, baada ya hapo alikuwa ofisa wa uchumi wa Shirika Tawala za Kiingereza-Kimarekani huko Magharibi mwa Ujerumani.
Mnamo mwaka wa 1949, alikuwa Katibu wa Uchumi akiwa chini Konrad Adenauer. Kuanzia mwaka wa 1957 hadi 1963, alikuwa Makamo wa Chansella. Baada ya Adenauer kujiuzulu mnamo mwaka wa 1963, Erhard akawa Chansela mpya wa Ujerumani. Mnamo mwaka wa 1966, Kurt Georg Kiesinger akampokea Bw. Ludwig Erhard.
Ludwig Erhard alikuja kufariki dunia mnamo mwaka wa 1977 mjini Bonn, Ujerumani.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.