From Wikipedia, the free encyclopedia
Lafarge ni kampuni ya viwanda ya Kifaransa iliyobobea katika vifaa vya ujenzi. Kwa sasa (2008) ni kampuni kubwa zaidi duniani ya kutengeneza saruji na kwa idadi iliyosafirishwa mbele ya Holcim.[2]
Makao Makuu | Paris, France |
---|---|
Mapato kabla ya riba na kodi | €3.362 billion (2008)[1] |
Profit | €1.598 billion (2008)[1] |
Tovuti | www.lafarge.com |
Lafarge ilianzishwa mwaka 1833 [3] na Joseph-Auguste Pavin de Lafarge katika mji wa Le Teil (Ardèche), kutumia mawe ya chokaa iliyo katika mji wa Mont Saint-Victor kati Le Teil na Viviers. Mawe ya chokaa ilikuwa nyeupe na 'argillaceous'} na ilitoa kwa kiasi kikubwa chokaa ya aina ya 'hydraulic lime'.
Mwaka 1864 Lafarge ilitia saini mkataba wake wa kwanza wa kimataifa ya utoaji wa tani 110.000 ya chokaa kwa mradi wa ujenzi wa Suez Canal [3] Ilitengeneza saruji za aina ya 'calcium aluminate'. Ilikuwa pia ni mwaanzilishi wa saruji nyeupe ya Portland, ambayo bado hufanywa katika kiwanda cha kwanza cha Le Teil cha kampuni.
Mwaka 1919, kampuni ya umma iliundwa, jina lake "Société anonyme des chaux et ciments de Lafarge et du Teil."
Mwaka 1980, ilijiunga na kampuni ya saruji ya Coppée na kuwa SA Lafarge Coppée.
Lafarge ilinunua kiwanda kutoka Kampuni ya Taifa ya Gypsum mapema-1987.[4] Miaka kumi baadaye, ilinunua Redland plc, kampuni ya marekani iliyoongoza katika kuendesha mashimo ya madini.
Mwaka 2001, Lafarge, kama kampuni ya pili kubwa zaidi ya saruji, ilinunua kampuni ya Blue Circle Industries (BCI), ambayo wakati huo ilikuwa kampuni ya sita kubwa zaidi ya saruji duniani, na kuwa kiongozi wa ulimwengu katika viwanda vya saruji [3]
Mwaka 2006, wanahisa wa Lafarge wa Amerika Kaskazini waliitikiaombi la bilioni $3 kutoka Kundi la Lafarge ambalo liliipa kampuni mzazi udhibiti kamili wa biashara ya Amerika ya Kaskazini, kuondoa LNA(Lafarge North America) kutoka Soko la Hisa la New York. Awali, kundi hilo lilimiliki asilimia 53% ya hisa za LNA [5]
Mwaka 2007, waliuza kiungo chao cha paa kwa kampuni ya kibinafsi katika mpango uliosababisha Lafarge kubakia na asilimia 35 ya hisa zake [3]
Mnamo Desemba 2007, Lafarge ilitangaza ununuzi wa kikundi cha saruji cha Orascom, iliyo na makao Misri,na iliyo na shughul Afrika nzima na 'Middle east', kutoka kwa Orascom Construction Industries (OCI) [6]
Tarehe 15 Mei 2008 Lafarge ilinunua Larsen & Turbo Ready Mix-Concrete (RMC) biashara nchini India kwa milioni $ 349.[7].
11 Julai 2008, gazeti la Albany Times Union lilitoa taarifa kwamba kiwanda cha Lafarge cha Ravena, New York "kilikuwa chanzo cha uchafu mwingi zaidi wa zebaki katika mji wa New York kutoka 2004-2006" [8] Kulingana na hadithi, mipango yalikuwa yamefanywa kuboresha kiwanda hicho ili kupunguza uchafu wa zebaki. Hadithi ya pili, iliyochapishwa siku iliyofuata, ilisema kuwa kiwanda hicho kilikuwa kimeto paundi 400 (kilo 181) za zebaki kila mwaka kutoka 2004-2006.[9]
Ifuatayo ni muhtasari wa takwimu:[1][10]
Takwimu za fedha katika mamilioni ya Euro | Mwaka | 2001 | 2002 | 2003 | 2004 | 2005 | 2006 | 2007 | 2008 |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mauzo | 13,698 | 14,610 | 13,658 | 14,436 | 15,969 | 16,909 | 17,614 | 19,033 | |
EBITDA | 2,862 | 3,101 | 2,820 | 3,028 | 2,920 | 3,610 | |||
Matokeo ya Ujumla | 750 | 446 | 728 | 868 | 1,096 | 1,372 | 1,909 | 1,598 | |
Madeni ya Ujumla | 9,332 | 8,544 | 6,734 | 7,017 | 7,221 | 9,845 | 8,685 | 16,884 | |
Wafanyikazi | 82,892 | 77,547 | 75,733 | 77,075 | 80,146 | 82,734 | 77,720 | 83,440 |
Washindani wakuu wa Lafage ni:
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.