La Verna
From Wikipedia, the free encyclopedia
La Verna, kwa Kilatini Alverna na kijiografia Monte Penna, ni mlima unaosimama peke yake hadi mita 1,283 katikati ya Apenini ya Toscana, juu ya bonde la Casentino, Italia ya Kati.
Ni maarufu hasa kwa sababu inasemekana Fransisko wa Asizi, akiwa kwenye mfungo mkali juu yake miezi ya Agosti na Septemba 1224, alipata njozi ya Yesu msulubiwa aliyemtia mwilini madonda yake matano.
Baadaye palijengwa patakatifu panapovutia watu wengi. Mnamo Agosti 1921 Papa Benedikto XV alipatangaza basilika dogo.[1]