Kurea
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kurea ni ndege wadogo wa nusufamilia Halcyoninae katika familia Alcedinidae. Spishi nyingine zinaitwa kichi au kijimbi-msitu. Wanafanana na midiria lakini ni wakubwa zaidi na spishi nyingi hutokea mbali na maji. Takriban spishi zote ni buluu mgongoni na domo lao ni jekundu mara nyingi. Spishi ndogo hula wadudu hasa lakini spishi kubwa zaidi hukamata kaa, vyura, mijusi, nyoka, panya au makinda ya ndege pia. Huchimba tundu katika ukingo wa mto, kichuguu au mti unaooza ambalo ndani lake jike huyataga mayai 2-5. Spishi nyingine zinatumia tundu la ndege mwingine kama zuwakulu au kigong'ota.
Kurea | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kurea kidari-kijivu | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||