From Wikipedia, the free encyclopedia
Kulungu mwekundu wa Atlas ni mnyama mkubwa wa jenasi Cervus katika familia Cervidae anayetokea Afrika ya kaskazini magharibi na visiwa vya Korsika na Sardinia. Zamani alifikiriwa kuwa nususpishi ya kulungu mwekundu wa Ulaya (Cervus elaphus barbarus), lakini wanyama wa Afrika wana mnasaba karibu na wale wa Korsika na Sardinia. Uchunguzi wa ADN unapendekeza kwamba wanyama hawa ni spishi tofauti.
Kulungu mwekundu wa Atlas | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kulungu mwekundu wa Atlas (Cervus corsicanus) | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Kulungu huyu ni mdogo kuliko yule wa Ulaya. Rangi ya mwili ni kahawia na kuna madoa meupe kwenye mbavu na mgongo. Hakuna tawi la pili juu ya pembe zake.
Spishi hii ni kulungu wa pekee wa Cervidae ambaye anatokea Afrika, katika misitu ya Aljeria, Maroko na Tunisia. Kuhusu nadharia moja watu wa zamani sana wamewasilisha spishi hii kwenye visiwa vya Korsika na Sardinia. Huko Maroko kulungu walimalizwa kwa uwindaji, lakini wanyama wengine waliwasilishwa kutoka Tunisia wakati wa miaka 1990[1]
Maadui wa kulungu mwekundu wa Atlas ni au walikuwa simba wa Barbari, dubu wa Atlas na chui wa Barbari, lakini wanyama hawa wamekwisha sasa au wamekuwa nadra.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.