![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/60/San_Trovaso_%2528Venice%2529_-_San_Cris%25C3%25B3gono_a_caballo_-_Michele_Giambono.jpg/640px-San_Trovaso_%2528Venice%2529_-_San_Cris%25C3%25B3gono_a_caballo_-_Michele_Giambono.jpg&w=640&q=50)
Krisogoni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Krisogoni (alifariki Aquileia, leo nchini Italia, 303 hivi) alikuwa mwanamume Mkristo wa Roma ya Kale ambaye aliuawa kwa sababu ya imani yake, inawezekana sana wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano[1].
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/60/San_Trovaso_%28Venice%29_-_San_Cris%C3%B3gono_a_caballo_-_Michele_Giambono.jpg/640px-San_Trovaso_%28Venice%29_-_San_Cris%C3%B3gono_a_caballo_-_Michele_Giambono.jpg)
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Wa kwanza wanaadhimisha sikukuu yake tarehe 24 Novemba[2], wa pili tarehe 22 Desemba (pamoja na anayesemekana alikuwa mwanafunzi wake Anastasia wa Sirmio).
Katika Martyrologium Hieronymianum aliorodheshwa katika tarehe mbili tofauti: 31 Mei na 24 Novemba[3]
Krisogoni ni kati ya watakatifu wanaotajwa katika Kanuni ya Kirumi.