From Wikipedia, the free encyclopedia
Krete (kwa Kigiriki Κρήτη, Kríti, matamshi ya kale, Krḗtē) ni kisiwa kikuu na chenye watu wengi zaidi cha Ugiriki, na ni cha tano katika Bahari ya Kati, baada ya Sicily, Sardinia, Cyprus na Corsica.
Pamoja na visiwa vya jirani vya bahari ya Aegean kinaunda mkoa wa Krete (Περιφέρεια Κρήτης), mmoja kati ya 13 ya nchi nzima. Mwaka 2011, mkoa huo ulikuwa na wakazi 623,065.
Mji mkuu na mji mkubwa ni Heraklion.
Krete ni sehemu muhimu ya ustaarabu na uchumi wa Ugiriki ukidumisha upekee wake katika utamaduni (kwa mfano upande wa ushairi na muziki).
Zamani (2700–1420 KK hivi) Krete ilikuwa kiini cha ustaarabu wa Minoa, wa kwanza kustawi huko Ulaya.[1]
Inatajwa na Biblia[2] pamoja na tabia za wakazi wake.
Katika miaka ya 60 Mtume Paulo alimuacha huko askofu Tito ili aweke wakfu mapadri katika kila mji. Halafu alimuandikia barua maarufu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.