Krak des Chevaliers
From Wikipedia, the free encyclopedia
Krak des Chevaliers (tamka: krak de she-va-lyee; kwa Kiarabu: قلعة الحصن Qalaat al-Husn) ni ngome ya kihistoria nchini Syria ambayo imeandikishwa katika orodha ya urithi wa dunia. Inapatikana juu ya mlima kwa kimo cha mita 600, takriban katikati ya mji wa Homs na pwani ya Bahari Mediteranea. Ilijengwa wakati wa vita za misalaba kama miaka 800 iliyopita ikawa kituo muhimu cha wanajeshi wa misalaba kutoka Ulaya.