Kiyangman
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiyangman kilikuwa lugha ya Kigunwingguan nchini Australia iliyozungumzwa na Wayangman katika jimbo la Northern Territory. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kiyangman, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiyangman kiko katika kundi lake lenyewe la Kiyangman. Wengine huiangalia kama lahaja ya Kiwardaman.