Kiwunumara
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwunumara kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wawunumara katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kiwunumara, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwunumara kiko katika kundi la Kimayabiki. Wengine hudai kwamba Kiwunumara ni lugha sawasawa na Kimayi-Kulan.