Kiwulna
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwulna (pia Kiwoolna au Kiwoolner) kilikuwa lugha ya asili nchini Australia iliyozungumzwa na Wawulna katika jimbo la Northern Territory. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kiwulna, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kiwulna kinafanyiza familia ya lugha pamoja na Kilimilngan; tena kinahusiana labda na Kiumbugarla na Kilaragiya.