Kiwikalkan
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwikalkan (pia Kiwik-Ngatharr au Kiwik-Alken) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wawik katika jimbo la Queensland. Mwaka wa 1981, idadi ya wasemaji wa Kiwikalkan ilihesabiwa kuwa watu 86 tu, na wasemaji wengi wameacha lugha yao ya kwanza na kutumia Kiwik-Mungkan. Kwa hiyo, Kiwikalkan imo hatarini mwa kutoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwikalkan kiko katika kundi la Kipama cha Kati. Wengine huiangalia kama lahaja ya Kiwik-Ngathana.