Kiwik-Mungkan
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwik-Mungkan ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wawik katika jimbo la Queensland. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kiwik-Mungkan ilihesabiwa kuwa watu 1060. Tena kuna watu 500 ambao hutumia Kimungkan kama lugha ya pili. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwik-Mungkan kiko katika kundi la Kipama cha Kati.