Kiwangkayutyuru
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwangkayutyuru kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wawangkayutyuru katika jimbo la Victoria. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kiwangkayutyuru ilitoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwangkayutyuru kiko katika kundi la Kikarniki. Wengine hukiangalia kuwa lahaja ya Kiwanggamala.