Kiwandarang
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kiwandarang kilikuwa lugha ya Kigunwingguan nchini Australia iliyozungumzwa na Wawandarang katika jimbo la Northern Territory. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kiwandarang, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwandarang kiko katika kundi la Kimara.