Kiwanda (lugha)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia Kiwanda (maana)
Kiwanda ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wawanda. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kiwanda imehesabiwa kuwa watu 24,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiwanda iko katika kundi la M20.