From Wikipedia, the free encyclopedia
Viunganishi ni neno au kikundi cha maneno chenye kuunganisha vipashio vya lugha ili kuunda kipashio kikubwa zaidi. Pia ni maneno yanayounganisha maneno mengine. Kiunganishi kinaweza kuunganisha neno na neno, kirai na kirai, kishazi na kishazi, sentensi na sentensi au vinginevyo.
Mifano |
---|
|
Viunganishi havina maneno ya kupambikwa katika neno au katika kupatanishwa kisarufi ndani ya tungo. Yaani, mfano cheza, chezewa, chezeka, na kadhalika. Hayo ni maumbo ya maneno ambayo hayabadiliki.
Na, lakini, ingawa, bila, au, ila, sembuse, kwa sababu, kwa kuwa, pamoja na, ijapokuwa, tena, iwapo, labda, toka, n.k.
Kuna aina mbili za viunganishi - navyo ni:
Ama:
Viunganishi huru ni vile vinavyosimama pekee katika tungo/katikati ya vipashio vinavyoungwa. Kwa mfano: Sisi tunaimba na kucheza.
Viunganishi tegemezi ni vile ambavyo huunda kwa viambishi vya o-rejeshi vinavyowekwa katika kishazi huru kwa pamoja huunda sentensi changamano. Viambishi hivyo ni kama vile: po, ye, lo, cho n.k. Kwa mfano: Mama anayepika ni msusi.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Viunganishi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.