Kisukari (samaki)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Visukari au haluwa ni samaki wadogo hadi wastani wa baharini wa jenasi Ariomma, jenasi pekee ya familia Ariommatidae katika oda Perciformes, wanaotokea maji ya kina kikubwa.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Kisukari | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kisukari fedha (Ariomma bondi) | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 7, 2 katika Afrika ya Mashariki:
| ||||||||||||||
Funga
Pezimgongo la visukari limegawanyika katika mapezi mawili. Lile la mbele lina miiba 10-12 na lile la nyuma lina tindi 14-18. Kuna mikuku minono miwili kila upande wa msingi wa mkia. Urefu wao ni sm 20-35 na kipeo cha sm 80 (kisukari mapezi-mafupi).