Kisotho-Kusini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kisotho-Kusini ni lugha ya Kibantu nchini Afrika Kusini inayozungumzwa na Wasotho. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kisotho-Kusini nchini Afrika Kusini imehesabiwa kuwa watu 4,240,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kisotho-Kusini iko katika kundi la S30.