Kisotho-Kaskazini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kisotho-Kaskazini (pia Kipedi) ni lugha ya Kibantu hasa nchini Afrika Kusini inayozungumzwa na Wasepedi. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kisotho-Kaskazini nchini Afrika Kusini imehesabiwa kuwa watu zaidi ya milioni nne. Pia kuna wasemaji 11,000 nchini Botswana. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kisotho-Kaskazini iko katika kundi la S30.