Kinyangga
lugha ya asili ya Australia iliyotoweka / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kinyangga (au Kiyangkaal) kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wanyangga katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kinyangga, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinyangga kiko katika kundi la Kitangiki. Wengine hukiangalia kuwa lahaja ya Kiganggalida.